Home » Articles » HEALTH

Entries in category: 34
Shown entries: 10-12
Pages: « 1 2 3 4 5 6 ... 11 12 »

Sort by: Date · Name · Rating · Comments · Views

UVUTAJI WA SIGARA NA TUMBAKU



Uvutaji wa sigara kama mazoea

Kama unavuta sigara kwa lengo la kukupoza pale unapohisi una msongo wa mawazo; kama hujisikii vizuri asubuhi mpaka upige pafu (uvute japo kidogo); kama unajisikia mfadhaiko, uchovu na kuumwa na kichwa ikiwa hujavuta sigara na pia ukajihisi kuwa huwezi kuzingatia jambo mpaka uvute sigara, basi ujue ya kwamba umetawaliwa sana na uvutaji wa sigara. Je kitu gani kinachofanya watu mpaka watawaliwe na uvutaji? Read More..........

HEALTH | Views: 1504 | Author: Yahyou M. Yahya | Added by: Admin | Date: 12/Jul/2013 | Comments (0)

MADHARA YA UVUTAJI WA SIGARA


Katika moshi wa sigara, zaidi ya kemikali 400 zimegundulika kuw ana madhara makubwa katika afya. Mvutaji mdogo hutumia nusu ya pakiti ya sigara kwa siku na kujikuta akiathiri mwili wake kwa kemikali hizi mara 3500 kwa  mwaka. Hata hivyo, vitu vitatu hatari zaidi katika sigara ni:

1.     Tar: hiki ni kisababisha kansa katika mwili.

2.   Nicotine:   Hiki ni kitu chenye sumu ambacho kwa muda mrefu san akimetumiwa kama dawa ya kuuwa wadudu na sumu ya panya. Inachukua nafasi ya pili kama sumu kali kabisa kwa athari yake mbaya katika mwili wa binadamu.

3.     Carbonmonoxide: Hii ni gesi inayopatikana katika moshi wa sigara.

Madhara mbalimbali ya vitu vinayopatikana katika moshi wa sigara ni kama yafuatayo: Read More.....


HEALTH | Views: 3141 | Author: Yahyou M. Yahya | Added by: Admin | Date: 12/Jul/2013 | Comments (0)

DHANA YA UKEKETAJI


Ni moja ya tatizo sugu sana linalowakabili wanawake katika jamii nyingi. Imekadiriwa ulimwengu mzima kuwa wanawake takriban milioni 120 wamekumbwa na tatizo hili.

Wanaounga mkono ukeketaji husema kuwa ni sehemu muhimu sana katika maisha ya kiutamaduni na kidini, na wengine hulinganisha na ile hali ya kutahiriwa mwanaume ambayo haipingwi hata kidogo na ni halali.

Lakini wale wanaopinga dhana ya ukeketaji husema kwamba, sio tu kwamba ukeketaji hutishia maisha ya wanawake, bali pia ni moja ya njia za unyanyasaji wa wanawake.

Katika baadhi ya nchi ambazo ukeketaji hufanyika sana utakuta ni kinyume na sheria – wale wanaong’ang’ania kufanya uchafu huu katika nchi hizo sasa wanaweza kushitakiwa na kufungwa, lakini bado hufanyika kimya kimya ndani ya familia na mbali na macho ya vyombo vya sheria. Soma zaidi..........

HEALTH | Views: 2601 | Author: Yahyou M. Yahya | Added by: Admin | Date: 16/Jun/2013 | Comments (0)